Uzinduzi
Nyanyuka Afrika Foundation

Kuinua Jamii na Kuleta
Maendeleo Endelevu

Tunalenga kumpa uwezo kijana na mwanamke kiuchumi, kulinda mazingira, na kuleta ustawi wa jamii kutoka Dodoma.

Mazingira
Ziara Yangu Mti Wangu

Kulinda Vyanzo vya Maji
na Kupanda Miti

Tunashirikiana na jamii katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia upandaji endelevu wa miti na kuzuia uchafuzi.

Dotto Stephen Masulubu

Mr. Dotto Stephen Masulubu

Mwanzilishi / Mkurugenzi Mkuu

Neno Kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu

"Nyanyuka Afrika Foundation ni taasisi ya kizalendo inayochochea mabadiliko chanya na fikra makini kwa vitendo hapa nchini Tanzania. Tunajikita katika kuwawezesha vijana na wanawake kiuchumi kupitia mitandao ya kibiashara, kutoa elimu ya uraia na msaada wa kisheria kwa wasio na uwezo, pamoja na kupambana na changamoto za tabianchi. Kupitia miradi yetu ya mazingira, tunalinda vyanzo vya maji na kuhamasisha upandaji miti endelevu ila kuhifadhi urithi wa vizazi vya sasa na baadae. Tunasimama imara kama daraja la maendeleo, tukiunganisha nguvu ya jamii, serikali na wadau mbalimbali kutoka makao makuu Dodoma hadi nchi nzima. Ungana nasi leo katika safari hii ya kuleta tabasamu, usawa vya kijamii na ustawi wa kudumu kwa kila Mtanzania."

Tunachokifanya kwa Vitendo

Our Impacts

Kupitia kujitolea, ushirikiano na wadau, tumefanikiwa kuleta mabadiliko chanya yanayoonekana katika jamii na mazingira yetu, na bado tunaendelea mbele.

0+

Miti Iliyopandwa

Kupitia kampeni ya "Ziara Yangu Mti Wangu" kulinda ikolojia na vyanzo vya maji.

0+

Vijana & Wanawake

Wamefikiwa na kuwezeshwa kiuchumi kupitia mitandao ya biashara na mafunzo.

0+

Msaada wa Kisheria

Wananchi waliopata uelewa wa haki zao kupitia kampeni zetu za kisheria mitaani.

Tunaendelea

Kila Siku

Kuongeza kasi ya miradi mipya ila kuwafikia watu wengi zaidi nchini kote.

Habari za Hivi Punde

News & Updates

Zote Zilizopita
Habari Matukio
June 2026

Uzinduzi wa Kikao cha Ziara na Mafunzo

Taasisi imefanya kikao kikubwa cha uzinduzi wa ziara na mafunzo maalum ya kiuchumi na kijamii mkoani Dodoma.

Habari Mazingira
June 2026

Kampeni ya "Ziara Yangu Mti Wangu" Yashika Kasi

Zoezi la ugawaji na upandaji miti limeendelea kwa mafanikio makubwa kwenye maeneo ya vyanzo vya maji.

Habari Urithi
May 2026

Mradi wa "Shitaka Urithi Mazingira"

Uhamasishaji wa jamii kuhusu utunzaji wa urithi wa asili na ulinzi wa wanyamapori dhidi ya uharibifu.

Inua Jamii, Tunza Kesho

Mchango Wako Ndio Injini ya Mabadiliko

Kila shilingi unayochangia inakwenda moja kwa moja kununua miche ya miti, kutoa mafunzo kwa vijana, na kuimarisha mitandao ya kiuchumi ya kina mama na wafanyabiashara wadogo hapa Tanzania.

Wanaofanikisha Safari Hii

Washirika Wetu / Partners

TFS Tanzania TFS Tanzania
NEMC NEMC
Dodoma Jiji Dodoma Jiji
Dulaiki Group Dulaiki Group

Ofisi na Posta

Cana Plaza, Dodoma | S.L.P 1249 Dodoma

Simu

+255 659 961 277 / +255 659 961 278

Barua Pepe

nyanyukaafrikafoundation@gmail.com